• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Iraq yalaani shambulizi la Iran kuvamia mamlaka yake

  (GMT+08:00) 2020-01-09 08:57:39

  Rais Barham Salih wa Iraq amelaani shambulizi la Iran, na kuzitaka pande mbalimbali zijizuie, kuzingatia kwanza mazungumzo na zisiiingize kanda hiyo kwenye vita.

  Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais wa Iraq inasema kuwa, rais Salih anafuatilia maendeleo ya hali katika kanda hiyo, kulaani Iran kufanya shambulizi la makombora dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani kwenye ardhi ya Iraq, amepinga kuvamiwa kwa mamlaka ya Iraq na kuifanya Iraq iwe medani ya vita kati ya pande mbalimbali.

  Taarifa hiyo pia inasema kuwepo kwa kikosi cha muungano wa kimataifa nchini Iraq kunatokana na makubaliano ya kupambana na ugaidi kati ya serikali ya Iraq na muungano wa kimataifa, kwa hiyo uwepo na hatma ya kikosi hicho pia ni mambo ya ndani ya Iraq.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako