• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Azam FC yamsajili Khleffin aliyekuwa kivutio cha kocha wao Cioaba

  (GMT+08:00) 2020-01-09 17:04:42

  Club ya Azam FC imekamilisha taratibu za kumsajili kiungo mshambuliaji Khleffin Hamdoun kutokea Mlandege FC ya Zanzibar kwa mkataba wa miaka minne. Huo ni usajili wa kwanza kwa Azam FC kwenye dirisha dogo la usajili, likiwa ni pendekezo la Kocha Mkuu, Aristica Cioaba. Hamdoun mwenye umri wa miaka 19, amesaini mkataba rasmi wa kuitumikia Azam FC Jumatano usiku, mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'. Mara baada ya kusaini mkataba huo, kiungo mshambuliaji huyo alielezea furaha yake ya kukamilisha taratibu ya kujiunga Azam FC huku akiahidi kushirikiana na wachezaji wenzake kuipa mataji timu hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako