• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa mambo ya nje wa China afafanua msimamo wa China kuhusu suala la Mashariki ya Kati

  (GMT+08:00) 2020-01-09 18:10:19

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yupo ziarani barani Afrika jana huko Cairo alipokutana na wanahabari pamoja na mwenzake wa Misri Sameh Shoukry, alifafanua msimamo wa China kuhusu masuala ya Mashariki ya Kati.

  Bw. Wang amesema, hivi karibuni mambo mengi yametokea katika kanda ya Masharki ya Kati, na hali ya wasiwasi imeongezeka kidhahiri. Hii inatokana na mivutano sugu ya kikanda, na pia ni matokeo ya vitendo vya upande mmoja, umwamba, maingilio ya kijeshi, na kupuuza kanuni na haki za kimataifa. Amesema China inatoa wito wa kuheshimu kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa na kusimamia ukweli, kutatua masuala kwa njia ya kisiasa, kufuata utaratibu wa pande nyingi, na kujenga kwa pamoja muundo endelevu wa usalama wa kikanda wenye ushirikiano na jumuishi, ili kutimiza utulivu na usalama wa nchi za Mashariki ya Kati kwa hatua za kivitendo.

  Bw. Wang amesema ikiwa mwenzi wa kimkakati wa nchi za Mashariki ya Kati, China itaendelea kuunga mkono kithabiti nchi hizo kulinda mamlaka, uhuru na ukamilifu wa ardhi, kujiendeleza kwa njia inayoendana na hali zao halisi, na kujitahidi kushirikiana kuhimiza amani na utulivu wa kikanda. China pia imekuwa, na itaendelea kuwa mjenzi wa amani wa Mashariki ya Kati, na kuhimiza utulivu na kuchangia maendeleo ya kanda hiyo.

  Kuhusu suala la Libya, Bw. Wang amesema China inaona mazungumzo ya kisiasa ni njia pekee ya kutatua suala hilo. Nchi za nje kuingilia suala hilo kwa njia ya kijeshi au kutumia nguvu ya kijeshi kunaweza tu kuongeza migogoro, na kulifanya suala hilo liwe gumu zaidi. Hivi sasa hali ya wasiwasi nchini Libya inaongezeka, makundi ya kigaidi ikiwemo ISIS yameharakisha kuingia nchini humo, na jumuiya ya kimataifa inapaswa kuwa na tahadhari. Ameongeza kuwa China inaunga mkono kusukuma mbele mchakato wa kisiasa nchini Libya chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa.

  Bw. Wang amesema, kati ya masuala yanayofuatiliwa, suala la Palestina halipaswi kupuuzwa tena, kwani wapalestina wanakumbwa na taabu kubwa. Utatuzi wa suala hilo ambalo limeendelea kwa zaidi ya miongo saba hauwezi kuahirishwa tena, na kuendelea kuwa mhanga wa "biashara" ya aina yoyote. Amesema China itaendelea kushikilia haki katika majukwaa mbalimbali ya kimataifa, kuendelea kuunga mkono Pendekezo la Amani lililotolewa na Nchi za Kiarabu, "Mpango wa Nchi Mbili", na kuunga mkono kujenga nchi huru ya Palestina yenye mamlaka kamili, mji mkuu wa Jerusalem ya mashariki, na mipaka iliyoamuliwa mwaka 1967.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako