• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachangia shughuli za kupambana na ugaidi duniani kwa juhudi za kuondoa msimamo mkali mkoani Xinjiang

    (GMT+08:00) 2020-01-09 18:11:00

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China imetoa mchango muhimu kwa vita ya dunia dhidi ya ugaidi kwa juhudi zake za kuondoa msimamo mkali mkoani Xinjiang.

    Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na mwenzake wa Misri Sameh Shoukry mjini Cairo, Wang amesisitiza kuwa suala la Xinjiang ni mambo ya ndani ya China, na kinachotokea Xinjiang ni suala la kupambana na mfarakano na ugaidi, sio suala la haki za binadamu au dini.

    Wang amesema kwa miaka mingi, mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur umeshuhudia maelfu ya matukio ya kigaidi ambayo yamesababisha vifo vya watu wengi wasio na hatia. Ili kulinda usalama wa watu wa makabila mbalimbali waishio mkoani Xinjiang, wakiwemo waislamu, kwa upande mmoja serikali ya China imepambana kithabiti na aina zote za shughuli za kigaidi, na kwa upande mwingine, imeanzisha vituo vya elimu na mafunzo ya ufundi stadi. Wang ameeleza kuwa vituo hivyo vinalenga kuwasaidia wale walioathiriwa vibaya na itikadi kali kwa kupitia elimu na mafunzo ya ufundi stadi ili kuondoa mzizi wa ugaidi.

    Wang ameongeza kuwa, katika kampeni ya kupambana na ugaidi mkoani Xinjiang, China imejifunza uzoefu wa nchi nyingi, ikiwemo Misri, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na nchi nyingine za magharibi kama vile Marekani na Ufaransa, na hatua hizo za China zimefuata sheria ipasavyo na zimetambuliwa kama ni hatua za kujikinga za kupambana na ugaidi.

    Wang amesisitiza kuwa juhudi za China za kupambana na ugaidi zimepata mafanikio na kwamba katika miaka mitatu iliyopita, Xinjiang haikushuhudia tukio lolote la kigaidi.

    Wang amesema wanafunzi wote katika vituo hivyo wamehitimu na kutokana na msaada wa serikali, wamepata ajira za kudumu na wanaishi maisha ya amani na usalama.

    Wang amesema uhuru wa kuamini dini ikiwemo Uislamu unalindwa ipasavyo mkoani Xinjiang, ambako kuna misikiti zaidi ya elfu 24, ambayo ni sawa na kila waislamu 530 wana msikiti mmoja, kiwango ambacho ni cha juu zaidi kuliko nchi nyingi za kiislamu.

    Wang amekosoa malengo mabaya ya baadhi ya nchi za magharibi zinazojaribu kuharibu utulivu wa Xinjiang na kuvuruga uhusiano kati ya China na dunia ya kiislamu kwa kupitia kuchafua jina la China ili kuzuia maendeleo yake. Amesisitiza kuwa nchi zinazokosoa China kuhusu suala la Xinjiang ni zile ambazo haziheshimu ustaarabu wa kiislamu na kusababisha vifo vya waislamu wengi wasio na hatia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako