• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Marekani aashiria kupunguza mvutano baada ya shambulizi la Iran kutokuwa na madhara

  (GMT+08:00) 2020-01-09 18:24:44

  Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa hakuna vifo wala majeruhi yaliyotokana na shambulizi la makombora lililofanywa na Iran jumanne wiki hii, akitoa ishara ya kupunguza mvutano lakini akitishia kuweka vikwazo vipya dhidi ya Iran.

  Rais Trump amesema hayo kwenye Ikulu alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu shambulio hilo, na kuongeza kuwa Marekani itaweka vikwazo zaidi vya kiuchumi kwa utawala wa Iran.

  Naye Waziri wa Ulinzi wa Marekani Mark Esper amewaambia wanahabari kuwa, kati ya makombora 16 ya masafa mafupi yaliyorushwa na Iran, 11 yalipiga kambi ya jeshi ya Ayn al-Asad na moja lilianguka karibu na kambi iliyopo Erbil.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako