• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uagizaji wa boda boda na tuk tuk (bajaji) nchini wafika Sh10 bilioni katika miezi tisa

  (GMT+08:00) 2020-01-09 19:18:15

  Uagizaji wa pikipiki maarufu kama bodaboda na tuk tuk au bajaji nchini Kenya, katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka jana ,uliongezeka kwa asilimia 26 kutoka kipindi sawa na hicho mwaka 2018.

  Takwimu kutoka Shirika la Taifa la Takwimu nchini Kenya (KNBS) zinaonyesha kuwa idadi ya jumla ya bodaboda na tuk tuk iliongezeka hadi 181,565 kutoka 143,966 katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka 2018.

  Ongezeko hilo lilifanya thamani ya uagizaji kwa ajili ya boda boda na tuk tuk kuongezeka kwa asilimia 28.7 hadi Sh10.3bn kutoka Sh8bn kipindi sawa na hicho mwaka 2018.

  Usafiri wa teksi wa boda boda na tuk tuk katika miaka ya hivi karibuni umeibuka kama sehemu kubwa ya uajiri kwa vijana wadogo walio mijini na maeneo ya vijijini ambao wameshindwa kupata kazi nyingine.

  Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa kufikia mwisho wa mwezi Disemba 2018 sekta hiyo ilikuwa imeajiri watu 258,900.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako