• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda-Bei za bidhaa zatarajiwa kuimarika

    (GMT+08:00) 2020-01-09 19:19:05
    Bei ya maharage nchini Rwanda imeshuka tangu kuanza kwa mkwa mpya baada ya kuwa juu mwishoni mwa mwaka jana.

    Kupanda huku kwa bei za bidhaa,haswa kati ya mwezi Oktoba na Disemba 2019,kulichangiwa na uhaba ulioshuhudiwa nchini humo na katika kanda.

    Ongezeko hilo katika bei za chakula liliongeza mfumuko wa bei hadi asilimia 6.9 kufikia mwezi Novemba,kutoka asilimia 4.4 mwezi Oktoba 2019,kiwango ambacho ni zaidi ya makadirio ya asilimia 5 ya Benki Kuu.

    Sasa hivi maharage ya ubora wa chini yanayojulikana kama Shyushya yanauzwa Rw600 kwa kilo kutoka Rw800 katika soko la Kimironko na maduka ya rejareja wilaya ya Kacyiru.

    Katika soko hilo hilo, maharage aina ya "coltan" ambayo yanachukuliwa kuwa ya ubora wa hali ya juu yanauzwa kwa Rw1,000 kwa kilo kutoka Rw1,200.

    Mkurugenzi wa Biashara ya ndani katika Wizara ya Biashara na Viwanda ,alisema maharage aina ya coltan yaliuzwa Rwf700 katika soko la Mulindi katika wilaya ya Gasabo kuanzia tarehe 5 Januari,na Rwf600 katika soko la Gahanga katika wilaya ya Kicukiro.

    Hata hivyo,bei za bidhaa nyingine haswa mahindi zipo juu-zikiwa kati ya Rwf500 na Rwf600 kwa kilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako