• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda-Ushuru wa umeme wapungua kwa asilimia 1.2

  (GMT+08:00) 2020-01-09 19:19:39
  Bei ya umeme nchini Uganda kwa miezi hadi kufika Machi imepunguzwa kwa asilimia 1.2. Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati (ERA) katika ushuru wa mwisho wa watumiaji umeme unaotumika kati ya Januari na Machi iliimarisha bei ya yuniti za kwanza za umeme katika Sh250. Punguzo dogo lilitekelezwa katika viwango vingine vya matumizi. Kwa mfano,watumiaji wa nyumbani sasa watalipa Sh751.7 kwa kila yuniti kutoka Sh752.5 mwaka jana huku watumizi wa biashara watalipa Sh649.4 kwa kila yuniti kutoka Sh666.1. Wateja wa viwanda vya viwango vya kati watalipa punguzo la Sh20.4 kutoka Sh595.6 hadi Sh575.2 huku wateja wa viwanda vikubwa watalipa Sh362.4 kutoka Sh364. Viwanda vikubwa zaidi sasa vitalipa Sh302.2 kutoka Sh302.6 kwa kila yuniti ya umeme iliyotumiwa.
  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako