• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maeneo ya Kihistoria Zanzibar yafanyiwe matengenezo ili yawe kivutio cha Utalii,Balozi Karume.

    (GMT+08:00) 2020-01-09 19:20:19
    Waziri wa Vijana,Utamaduni,Sanaa na Michezo Zanzibar,Balozi Ali Karume,ameushauri uongozi wa Idara ya Habari,Utalii, na Mambo ya Kale Zanzibar kuyafanyia matengenezo maeneo ya kihistoria ili yawe kivutio cha utalii.

    Alisema kwa muda mrefu maeneo ya kihistoria yalikosa kufanyiwa ukarabati na kupelekea kukiosesha serikali mapato.

    Akizungumza katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi vyumba vya kihistoria ya Wareno eneo la Fukuchani Mkoa wa Kaskazini Unguja ,Balozi Karume alisema maeneo ya kihistoria yanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi iwapo miundombinu yake itafanyiwa ukarabati na kuwa kivutio cha utalii.

    Alisema serikali ya Dk.Ali Mohamed Shein imeweka mikakati ya kuyafanyia marekebisho maeneo ya kihistoria ili kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini humo.

    Aidha aliwaomba wananchi ,taasisi binafsi,shehia na wanafunzi kushirikiana na Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale katika kuyalinda na kuyatunza maeneo hayo ili yaweze kuwa endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako