• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Iran yasema ajali ya ndege ya Ukraine ilitokana na sababu za kiufundi

  (GMT+08:00) 2020-01-10 08:44:22

  Waziri wa barabara na maendeleo ya miji wa Iran Bw Mohamed Eslami amesema ajali ya ndege ya Ukraine ilitokana na dosari za kiufundi na amepuuza uvumi kuwa ajali hiyo ilitokana na urushaji wa makombora ya Iran dhidi ya vituo vya kijeshi vya Marekani nchini Iraq.

  Bw. Eslami amekanusha uvumi kuwa kulikuwa na shambulizi la kigaidi, mlipuko au ufyatuaji wa risasi kwenye ndege ambao umesababisha ajali hiyo, lakini uvumi huo wote si kweli.

  Hata hivyo habari kutoka Ottawa Canada zinasema waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Justin Trudeau amesema serikali yake ina taarifa za kijasusi zinazoonesha kuwa ndege hiyo ilitunguliwa kwa kombora lililorushwa kutoka ardhini. Kauli ya Bw. Trudeau imekuja wakati vyombo vya habari nchini Marekani vinasema maofisa wa Marekani wanaamini kuwa ndege hiyo ilitunguliwa kwa bahati mbaya na makombora ya Iran.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako