• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jeshi la mashariki mwa Libya lakataa mwito wa Uturuki-Russia kusimamisha mapambano

  (GMT+08:00) 2020-01-10 08:44:46

  Jeshi la Libya lenye makao yake makuu kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo limekataa mwito wa marais wa Uturuki na Russia kusimamisha mapambano haraka mjini Tripoli.

  Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo inasema jeshi hilo litaendelea kupambana na makundi ya kigaidi, na hakuna njia ya kuanzisha nchi iliyotulia bila kuwaangamiza.

  Serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa na baraza la juu la Mjini Tripoli wamekaribisha mwito wa Uturuki na Russia kusimamisha mapambano, na kusema wako tayari kukomesha mapambano na kuanza mchakato wa kisiasa.

  Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa nchini Libya Bw Ghassan Salame amekaribisha mwito huo, na kutaka pande mbili ziitikie mwito huo na kukomesha shughuli za kijeshi mara moja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako