• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • FAO yasema bei za chakula duniani zimepanda kufikia kiwango cha juu zaidi katika miaka mitano iliyopita

  (GMT+08:00) 2020-01-10 09:34:15

  Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema, bei za chakula duniani zimepanda mwezi wa Desemba mwaka jana na kufikia kiwango cha juu zaidi katika miaka mitano iliyopita.

  Ongezeko hilo jipya linaashiria kumalizika kwa mwaka ambao kigezo cha bei za chakula cha shirika hilo kinapanda na kushuka. Bei hizo zimepanda katika miezi mitano ya mwanzo huku zikishuka katika miezi mitatu inayofuata kabla ya kuongezeka kwa miezi minne inayofunga mwaka huu.

  Mwezi wa Desemba mwaka jana, kigezo hicho kimeongezeka kwa asilimia 1.5 ikilinganishwa na mwezi wa Novemba, ambacho kimeongezeka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na mwanzoni mwa mwaka huu na kufikia kiwango cha juu zaidi tangu mwezi wa Desemba mwaka 2014.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako