• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lahimiza nchi wanachama wote kufuata Katiba ya Umoja wa Mataifa

  (GMT+08:00) 2020-01-10 09:45:23

  Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa jana limetoa taarifa ikiwataka nchi wanachama kufuata Katiba ya Umoja wa Mataifa, na kusisitiza kuwa baraza hilo linajitahidi kulinda taratibu za pande nyingi na hadhi muhimu ya Umoja wa Mataifa katika mambo yanayohusisha pande nyingi.

  Baraza la usalama limepitisha taarifa kwenye mjadala wa ngazi ya juu kuhusu "kufuata Katiba ya Umoja wa Mataifa, kulinda amani na usalama wa kimataifa".

  Mjumbe wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amehudhuria mjadala huo na kueleza msimamo wa China. Amesema China ilikuwa nchi ya kwanza kusaini Katiba ya Umoja wa Mataifa, na inatimiza ahadi zake, kushikilia kutatua mgogoro kwa njia ya amani, kuheshimu usawa wa mamlaka, uhuru wa siasa na ukamilifu wa ardhi wa nchi mbalimbali, kutoingilia mambo ya nchi nyingine, na kutotumia au kutotishia kutumia nguvu. China pia itatekeleza wajibu wake kwenye katiba hiyo, kushiriki kwenye operesheni ya kulinda amani, kutekeleza wajibu wa kifedha, kuunga mkono Umoja wa Mataifa kuchukua nafasi muhimu katika mambo ya kimataifa. China itajitahidi kutekeleza ajenda ya mwaka 2030 ya Umoja wa Mataifa, kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kwa ubora, ili maendeleo ya China yanufaishe nchi mbalimbali duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako