• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Yanga yawanyima raha mashabiki baada ya kutolewa kwa penalti na Mtibwa Sugar kombe la mapinduzi

  (GMT+08:00) 2020-01-10 12:57:37

  Timu ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa penalti 4-2 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 jana usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Kipa wa tatu wa Yanga, Ramadhani Awam Kabwili alipangua penalti ya kiungo Abdulhalim Humud 'Gaucho', lakini wenzake beki Kelvin Yondani akagongesha mwamba na kiungo Abdulaziz Makame akapiga juu ya lango. Waliofunga penalti za Mtibwa Sugar ni Omary Sultan, Dickson Job, Jaffary Kibaya na Shomari Kibwana na za Yanga zilifungwa na beki Paul Godfrey 'Boxer' na kiungo Mapinduzi Balama 'Kipenseli'. Awali, Yanga SC ilitangulia kwa bao la kiungo wake mshambuliaji, Deus David Kaseke dakika ya 36 na Mtibwa Sugar ikasawazisha dakika ya 90 kupitia Shomari Kibwana. Nusu Fainali nyingine itafuatia leo kwa mchezo baina ya mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC dhidi ya washindi wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Azam FC Saa 2:15 usiku hapo hapo Uwanja wa Amaan, wakati fainali itafanyika Jumapili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako