• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UOGELEAJI: Fina yalisimamisha Shirikisho la Uogeleaji la Kenya (KSF) kwa kutofanya uchaguzi

  (GMT+08:00) 2020-01-10 12:59:07

  Ushiriki wa waogeleaji wa kenya kwenye michezo ya Olimpiki ya Tokyo upo njia panda baada ya Shirikisho la Uogeleaji la Kimtaifa Fina kulisimamisha Shirikisho la Uogeleaji la Kenya (KSF) hadi litakapofanya uchaguzi. KSF mara ya mwisho ilifanya uchaguzi mwaka 2014 lakini licha ya kukumbushwa mara kwa mara na Fina, wameshindwa kuchaguza viongozi wapya, na kupelekea Fina kuchukua hatua hiyo. Mara ya kwanza Fina iliipa Kenya tarehe ya mwisho kufanya uchaguzi ambayo si zaidi ya Juni 30, 2019, na kuongezewa muda kwa mara ya pili ambao si zaidi ya Oktoba 30, 2019 hata hivyo Fina iliendelea kuwa na huruma na kuipa hadi Novemba 30. Juu ya yote hayo muda wa mwisho haukufikiwa na KSF na hakuna uchaguzi wowote uliofanyika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako