• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • VOLIBOLI UFUKWENI: Rwanda yaelekea Tanzania kushiriki michuano ya sub-Zone 5 ya kufuzu Olimpiki ya Tokyo 2020

  (GMT+08:00) 2020-01-10 12:59:40

  Timu za taifa za mpira wa wavu wa ufukweni kwa akina dada za Rwanda zimeondoka jana nchini kuelekea Dar es Salaam, Tanzania, kushiriki michuano ya raundi ya kwanza ya kufuzu michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020. Michuano hiyo ya kufuzu ya kanda sub-Zone 5 inaanza leo na kumalizika Jumapili, huku timu mbili za juu zikiendelea raundi inayofuata ambayo itachezwa mwezi ujao. Timu za Christophe Mudahinyuka zinaonekana kuwa na uwezo mkubwa kwenye kundi ambalo pia lina timu za Uganda, Kenya na wenyeji Tanzania. Rwanda itawakilishwa na timu mbili, timu ya kwanza ikiwa na wachezaji Charlotte Nzayisenga na Valentine Munezero na timu ya pili ikiwa na Seraphine Mukantambara na Judith Hakizimana

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako