• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi awatunuku wasomi wawili tuzo ya juu ya sayansi ya China

  (GMT+08:00) 2020-01-10 15:48:50

  Rais Xi Jinping wa China amewatunuku Huang Xuhua na Zeng Qingcun tuzo ya juu ya sayansi ya China ili kupongeza mchango wao mkubwa kwenye sayansi na ubunifu wa kiteknolojia.

  Huang Xuhua, msomi wa Taasisi ya Uhandisi ya China ni msanifi mkuu wa nyambizi ya nyuklia ya kizazi cha kwanza ya China. Huang alizaliwa mwaka 1926 na amejishughulisha na utafiti na utengenezaji wa nyambizi za nyuklia kwa miaka karibu 30.

  Zeng Qingcun, mwenye umri wa miaka 85 ni mtaalam maarufu wa hali ya hewa kutoka kitengo cha utafiti wa hali ya hewa na fizikia kilicho chini ya Taasisi ya Sayansi ya China. Nadharia yake ya utabiri wa hali ya hewa kwa mujibu wa mahesabu imetatua matatizo ya kwenda na wakati na utulivu katika kuhesabu mabadiliko ya hali ya hewa ya viwango tofauti, pia ni msingi wa teknolojia ya utabiri wa hali ya hewa kwa mujibu wa mahesabu duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako