• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito wa kudumisha amani na utulivu katika Mashariki ya Kati

    (GMT+08:00) 2020-01-10 17:09:43

    Mwanadiplomasia wa wizara ya mambo ya nje ya China, Balozi Qi Qianjin alipokutana na wanahabari wa China na Israel mjini Tel Aviv, Israel, amefafanua maoni ya China kuhusu uhusiano kati yake na Israel na masuala yanayofuatiliwa zaidi ya Mashariki ya Kati. Amesema China inatumai kuwa kanda hiyo inaweza kudumisha amani na utulivu, na uhusiano kati ya China na Israel utaendelea kwa utulivu.

    Bw. Qi amesema hivi karibuni alikutana na baadhi ya maofisa na wasomi wa Israel, na wanaona kuwa uhusiano kati ya China na Israel katika sekta za uchumi, biashara, sayansi na mawasiliano ya watu na ustaarabu umeendelea na kuwa wa kiwango cha juu. Anasema,

    "Serikali ya China inafurahia kuona mafanikio ya uhusiano kati ya nchi hizi mbili, na serikali na watu wa China wangependa kuinua zaidi kiwango cha uhusiano huo. Nafurahia kuwa Israel imethibitisha uhusiano huo kuwa imara, na hautaathiriwa na pande nyingine na matukio mengine. Kuendeleza uhusiano kati ya Israel na China ni sera ya wazi na endelevu ya China."

    Balozi Qi amesema China inafuatilia kwa karibu mgogoro kati ya Marekani na Iran ambao umesababisha hali ya wasiwasi katika kanda ya Mashariki ya Kati, na kuzitaka nchi hizo zijizuie. Anasema,

    "Tunaona kuwa maendeleo ya hali ya Mashariki ya Kati yataleta athari kubwa kwa kanda hiyo na dunia nzima. Migogoro na vita itaathari maslahi ya China na nchi nyingine nyingi, hivyo tunatumai kuwa nchi za kanda hiyo ikiwemo Israel na Iran zitajituliza, na kuendelea kutafuta njia ya kupunguza hali ya wasiwasi."

    Balozi Qi amesema mivutano ya Mashariki ya Kati inatokana na sababu mbalimbali za kihistoria, Misri, Syria na Iraq zilikuwa viongozi wa Mashariki ya Kati, na hivi sasa Israel, Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na Iran zimejitokeza na kuwa nchi muhimu za kanda hiyo, na hali hii imeleta mabadiliko ya kisiasa. Kwa upande mwingine, tangu Donald Trump aingie madarakani, Marekani imebadilisha sera yake ya kidiplomasia kuhusu masuala ya Mashariki ya Kati, na kuleta utatanishi mkubwa. Anasema,

    "Naona kuwa kanda ya Mashariki ya Kati itakabiliwa na hali tatanishi zaidi, kwani uwiano wa nguvu za kisiasa za pande mbalimbali haupatikani kwa urahisi. Hii inamaanisha kuwa nchi zote za kanda hiyo ikiwemo Israel, Saudi Arabia na Iran zinapaswa kutafuta njia ya kulinda amani na utulivu wa kikanda. Licha ya hayo, Marekani ambayo ni nguvu muhimu inayoingilia masuala ya Mashariki ya Kati inapaswa kufanya kazi chanya katika kuhimiza amani na kujenga mifumo husika."

    Aidha, Balozi huyo pia amezungumzia changamoto za ukarabati wa Syria, msimamo wa China kuhusu suala la Israel na Palestina ambao ni kushikilia mpango wa nchi mbili, na kutatua suala hilo kwa njia ya mazungumzo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako