• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Msimu wa safari nchini China waanza wakati sikukuu ya Spring ikikaribia

  (GMT+08:00) 2020-01-10 18:29:37

  Msimu wa safari nchini China umeanza leo, ikiwa ni siku 15 kabla ya sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China.

  Makadirio yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Mageuzi na Maendeleo yameonyesha kuwa, kutakuwa na safari bilioni 3 wakati wa msimu wa safari kuanzia Januari 10 hadi Februari 18, ikiwa ni ongezeko kidogo ikilinganishwa na mwaka jana.

  Tume hiyo pia imekadiria ukuaji wa asilimia 8 katika safari za treni, asilimia 8.4 kwa safari za anga, na asilimia 9.6 kwa safari za baharini.

  Mwaka Mpya wa Jadi wa China unaangukia Januari 25 mwaka huu, ikiwa ni mapema zaidi kuliko miaka iliyopita, na kuleta changamoto kunwa kwenye mfumo wa usafiri kutokana muda wa vyuo kufunguliwa kuingilia na msimu huo wa safari.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako