• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yazitaka pande zote zinazohusika kushiriki kwenye uchunguzi wa ajali ya ndege ya Ukraine

    (GMT+08:00) 2020-01-10 18:30:03

    Iran imezitaka pande zote zinazohusika kuchangia katika uchunguzi wa ajali ya ndege ya Ukraine iliyosababisha vifo vya watu 176 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

    Ndege hiyo ya abiria aina ya Boeing 737-800 ni mali ya Shirika la Ndege la Kimataifa la Ukraine na ilianguka karibu na Uwanja wa Kimataifa wa Imam Khomenei muda mfupi baada ya kuruka. Ajali hiyo imetokea wakati mvutano kati ya Marekani na Iran ukiendelea. Jumanne wiki hii, Iran ilirusha makombora kwenye kambi za jeshi za Iraq zenye askari kutoka Marekani, ikiwa ni kujibu kitendo cha Marekani cha kumuua jenerali wa ngazi ya juu wa Iran wiki iliyopita.

    Maofisa wa Marekani wanaamini kuwa ndege hiyo ilitunguliwa kwa bahati mbaya na Iran, huku mamlaka nchini Iran zikisisitiza kuwa ajali hiyo imetokana na matatizo ya kiufundi, na kupuuza madai kuwa ni shambulizi la kigaidi.

    Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amesema jana kuwa nchi hiyo iko tayari kushiriki kwenye uchunguzi kuendana na sheria za kimataifa, na kwamba kundi la wataalam wa Ukraine wamewasili Iran jumatano na watafanya uchunguzi katika eneo la ndege hiyo ilipoanguka. Iran pia imeialika Bodi ya Usalama wa Safari ya Marekani kushiriki kwenye uchunguzi huo. Bodi hiyo leo imesema, itashiriki kwenye uchunguzi wa ajali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako