• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Liverpool yamwinda Mbappe

  (GMT+08:00) 2020-01-10 18:36:42

  Baada ya Liverpool kusaini dili nzito na kampuni ya Nike kwa mkataba unaoweza kuiletea klabu hiyo Sh10 bilioni kila mwaka, The Reds imepata nguvu za kumtwaa kinda mahiri wa PSG, Kylian Mbappe. Habari nyingine zinasema, timu kadhaa za Uingereza ikiwemo Manchester United zimeingia vitani kuwania saini ya kiungo mshambuliaji mahiri, Edison Cavani wa Paris Saint-Germain (PSG). Straika huyo mwenye umri wa miaka 32 amecheza mechi nne pekee za Ligi Kuu ya Ufaransa msimu huu baada ya kusumbuliwa na jeraha mbali na kukosa namba kutokana na upinzani mkali kutoka kwa Mauro Icardi. Mkataba wake na PSG unamalizika mwishoni mwa msimu huu na sasa anatarajiwa kuwa huru iwapo atakataa mkataba mpya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako