• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • VOLLEYBALL: Rais Uhuru apongeza Malkia Strikers baada ya kufuzu Olimpiki

  (GMT+08:00) 2020-01-10 18:37:16

  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amepongeza timu ya wanawake ya Volleyball ya nchi hiyo Malkia Strikers kwa kufuzu kuingia kwenye mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo, Japana. Timu hiyo ilifuzu baada ya kuinyuka Nigeria seti tatu kwa nunge. Akina dada hao wa Kenya waliingia kwenye mashindano ya Afrika kufuzu kwenye Olimpiki na kuzishinda timu zote walizokutana nazo. Waliwachapa Misri 3-1, Botswana 3-0, Cameroon 3-2, kabla ya kuwashinda Nigeria k na kuibuka washindi. Rais Kenyatta amesema ushindi wa timu hiyo kwenye mechi hizo zilizosakatwa Cameroon ni ishara tosha Kenya inazidi kutamba kispoti

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako