• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kiongozi wa mkoa wa Hong Kong akutana na mkurugenzi mpya wa ofisi ya mawasiliano ya serikali kuu ya China katika mkoa huo

  (GMT+08:00) 2020-01-10 18:41:05

  Kiongozi wa mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong Bibi Carrie Lam amekutana na mkurugenzi mpya wa ofisi ya mawasiliano ya serikali kuu ya China katika mkoa huo Bw. Luo Huining.

  Bibi Lam amemjulisha Bw. Luo kazi za serikali ya Hong Kong katika sekta mbalimbali ndani ya miaka miwili iliyopita na msukosuko wa kijamii kutokana na mabadiliko ya sheria. Pande hizo mbili zimeona kuwa, katika miezi 7 iliyopita, Hong Kong imekabiliwa na hali ngumu zaidi tangu irudi China, na athari kubwa kwa pande mbalimbali za jamii. Bibi Lam amesema, serikali ya Hong Kong itafuata sheria ya msingi na sera ya Nchi Moja Mifumo Miwili, kuzuia mapambano, kulinda utekelezaji wa sheria na kuiwezesha Hong Kong itatue mgogor uliopo. Pande hizo mbili zina imani kuwa, Hong Kong inaweza kufungua ukurasa mpya mzuri na kujiunga kwenye maendeleo ya China ili kutimiza ustawi na utulivu wa kudumu chini ya uungaji mkono wa serikali kuu ya China.

  Bibi Lam pia amesema, hivi sasa, hali ya kiuchumi ya Hong Kong si nzuri, na serikali itajitahidi kuchukua hatua kusaidia watu kuondokana na matatizo yaliyopo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako