• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 15 wa mazungumzo ya kimkakati kati ya China na Japan kufanyika mjini Xi'an, China

    (GMT+08:00) 2020-01-10 18:41:34

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, mkutano wa 15 wa mazungumzo ya kimkakati kati ya China na Japan utafanyika tarehe 14, mwezi huu, mjini Xi'an, China.

    Bw. Geng amesema, naibu waziri wa mambo ya nje ya China Bw. Le Yu atazungumza na mwenzake wa Japan Bw. Takeo Akiba na kubadilishana maoni kuhusu uhusiano wa pande mbili na masuala yanayofuatiliwa kwa pamoja ya kimataifa na ya kikanda.

    Bw. Geng amesema, hivi sasa, mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa mzuri. China inatarajia pande hizo mbili zitachukua fursa hiyo kuendelea kuongeza makubaliano na uaminifu na kujenga mazingira mazuri kwa kutekeleza mchakato wa mambo makubwa ya kisiasa ya pande mbili na kusukuma mbele maendeleo ya uhusiano kati yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako