• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Lamu ni salama kwa uwekezaji

  (GMT+08:00) 2020-01-10 19:17:39
  Serikali ya kaunti ya Lamu na ile ya kitaifa, zimewarai wawekezaji kupuuzilia mbali matukio ya hivi maajuzi ambapo, eneo hilo lilikumbwa na mashambulio, na badala yake kuzuru Lamu na kuwekeza kwenye miradi mbalimbali.

  Gavana wa Lamu, Fahim Twaha, Kamishna wa Kaunti hiyo Irungu Macharia na Kamanda wa Polisi eneo hilo, Muchangi Kioi, wamesema Lamu kwa sasa imedhibitiwa vilivyo kiusalama na kwamba wawekezaji, watalii na wanabiashara wengine wako huru kuzuru eneo hilo wakati wowote ili kuendeleza azma yao ya maendeleo.

  Katika kikao cha jumla na wanahabari kwenye makao makuu ya Kaunti ya Lamu mjini Mokowe mnamo Jumatano, viongozi hao pia waliwataka wakazi eneo hilo kuondoa shaka na badala yake kuelekeza fikra zao katika kujiendeleza maishani.

  Bw Twaha aliwashukuru walinda usalama kwa juhudi zao katika kuhakikisha amani na utulivu vinarejea eneo hilo.

  Alisema serikali yake itaendelea kushirikiana kwa karibu na idara ya usalama ili kuona kwamba amani na utulivu vinadumishwa Lamu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako