• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vita vya Iran na Marekani kuathiri mkenya wa kawaida.

  (GMT+08:00) 2020-01-10 19:18:01
  Wasiwasi umezuka nchini Kenya kuhusu uwezekanao wa mzozo kati ya Iran na Amerika kuathiri hali ya maisha ya wakenya.

  Kwa mujibu wa wataalamu wa kiuchumi na usalama, kuna uwezekano mkubwa Kenya kuathirika baada ya utawala wa Rais Donald Trump kumwangamiza Luteni Jenerali Qasem Soleimani wa Iran wiki iliyopita.

  Hii ni kwa sababu ya ushirikiano wa karibu kati ya Kenya na Amerika katika nyanja tofauti, na pia kutatizika kwa usafirishaji wa mafuta na uuzaji wa bidhaa za kilimo nchini Iran.

  Soleimani alikuwa kamanda wa kijeshi Iran, na aliuawa kwa bomu la Amerika kwenye msafara wake katika uwanja wa ndege jijini Baghdad, Iraq.

  Athari ya kwanza kuu inayotarajiwa ni ongezeko la bei ya mafuta, ambayo itaathiri bei ya bidhaa zingine vikiwemo vyakula.

  Bei ya mafuta ulimwenguni ilipanda kwa asilimia mbili na huenda ikazidi kupanda kadri mzozo huo unavyoendela kuzorota. Ukanda wa Mashariki ya Kati hutegemewa zaidi ulimwenguni kwa uzalishaji mafuta na wakati unapozuka mzozo kama huu uliopo kwa sasa, bei ya mafuta hupanda.

  Sekta ya kilimo cha majani chai pia imeanza kuingiwa wasiwasi, kwani Iran ni mnunuzi mkubwa wa zao hilo kutoka Kenya.

  Wahusika katika sekta hiyo jana walisema vitisho vya Iran kwamba italipiza kisasi kutokana na mauaji ya Soleimani huenda ikawatia hofu wafanyabiashara wanaouza majani chai ya Kenya nchini humo. Iran ilinunua kilo 532,715 za majani chai ya Kenya mwaka jana. Kenya huuza takriban asilimia 20 ya majani chai kwa taifa hilo la ukanda wa Mashariki ya Kati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako