• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan yafungua soko la dhahabu ili kuongeza mapato yake

  (GMT+08:00) 2020-01-10 19:19:51

  Kwa muda mrefu Benki kuu ya Sudan imekuwa ikinunua dhahabu kutoka kwa wafanyibiashara nchini humo na kuiuuza nje ili kupata fedha za kigeni. Hata hivyo, katika hatua ya hivi punde, wizara ya Hazina ya kitaifa imewaruhusu wafanyibiashara nchini Sudan kuuza dhahabu kwa mataifa mengine ili kuikwamua wizara hiyo kuokana na uchache wa fedha za kuendesha shughuli za serikali.

  Kaimu gavana wa benki kuu ya Sudan Badral-Din Abdel Rahim, amenukuliwa akisema kwamba benki kuu haitajihusisha tena na shughuli ya kuuza na kununua dhahabu. Juma lililopita, kampuni moja ya kibinafsi ilitumia fursa hii kuuza kilo 155 za dhahabu nje ya taifa la Sudan.

  Serikali ya Sudan kupitia Wizara ya Hazina ya Kitaifa, imechukuwa hatua hii ili kukusanya pesa zaidi kuisaidia katika shughuli zake za kila siku, ikizingatiwa kwamba sasa, Sudan inakumbwa na wakati mgumu kiuchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako