• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashiriki katika mageuzi ya kiuchumi ya nchini Djibouti

    (GMT+08:00) 2020-01-10 19:36:57

    Wakati Djibouti inatumia kwa kikamilifu fursa kubwa ya kiuchumi inayotokana na eneo lake la kimkakati la kijiografia, ushiriki wa China umesaidia matarajio ya nchi hiyo kuwa nchi muhimu kiuchumi, katika biashara na pia mambo ya bahari, ikiunganisha bara la Afrika na Bahari Nyekundu. China imesaidia mageuzi ya Djibouti kupitia ushiriki wake katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli yenye urefu wa kilomita 752 inayoanzia bandari ya Djibouti hadi mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

    Kutokana na eneo muhimu la kijiografia, Djibouti, iliyoko kwenye pwani ya Bahari Nyekundu katika Ghuba ya Aden na inaunganisha mabara matatu ya Afrika, Asia, na Ulaya, inatumika kama ufunguo muhimu wa ushoroba wa baharini na kituo cha kibiashara, na hii inatokana na Eneo la Biashara Huria la Kimataifa la Djibouti lililojengwa na China, pamoja na miradi mingine mbalimbali ya miundombinu ya kisasa.

    Rais wa Djibouti Ismael Omar Guelleh anasema, umuhimu wa Eneo hilo unakwenda mbali zaidi ya kanda ya IGAD na kufikia bara zima la Afrika, kama alivyosema rais wa Rwanda Paul Kagame, kwamba miundombinu muhimu sio tu itaisaidia Djibouti, lakini eneo pana zaidi la bara la Afrika.

    Ushirikiano na China pia umeisaidia Djibouti kuwa na bandari mpya ya kisasa. Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na Mamlaka ya Bandari na Eneo Huria la Djibouti zimeonyesha kuwa, biashara ya ndani na nje ya nchi hiyo kupitia bandari za Djibouti imeongezeka katika miaka ya karibuni. Hii inatokana na maendeleo ya miundombinu kama vile bandari ya Doraleh iliyojengwa na China na kuzinduliwa rasmi Mei mwka 2017. Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo Aboubaker Omar Hadi ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kuwa, Mamlaka hiyo imefanya biashara ya ndani na nje yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 41. Amesisitiza kuwa mafanikio hayo yasingefikiwa bila ya maendeleo sahihi ya miundombinu, kama vile bandari na njia za reli.

    Hivi sasa, Ethiopia na Djibouti zinaadhimisha miaka miwili tangu reli ya SGR inayoziunganisha nchi hizo mbili ianze kufanya kazi Januari mwaka 2018. Reli hiyo yenye umbali wa kilomita 725 ilijengwa na kampuni ya China, na ni reli ya kwanza ya umeme inayounganisha nchi mbili barani Afrika.

    Akizungumza na shirika la habari la China, Xinhua, mshauri mkuu kwenye Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa kuhusu pendekezo la Ushirikiano kati ya Kusini na Kusini Gedion Jalata amesisitiza kuwa reli hiyo imekuza kwa pande zote uchumi wa Ethiopia na Djibouti kwa pamoja.

    Ushirikiano unaopanuliwa kati ya China na Djibouti umeiwezesha Djibouti kutumia vizuri manufaa yanayotokana na idadi ya watu, haswa kwa kupitia kutoa maelfu ya ajira nzuri kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi.

    Vilevile, China imeisaidia Djibouti kujenga uwezo na kusafirisha ujuzi wake kwa kupitia kutoa fursa za elimu na mafunzo kwa vijana wa nchi hiyo katika sekta mbalimbali, kutuma wataalam wa China nchini Djibouti pamoja na kuwawezesha watu wa Djibouti katika maendeleo makubwa ya kiteknolojia.

    Wakati Djibouti inapotekeleza mipango yake mipya ya kuhimiza maendeleo ya teknolojia ambayo hayapatikani kwa urahisi kwa nchi hiyo, ushiriki wa China katika maendeleo ya uwezo umetoa mchango mkubwa katika kuisaidia kuziba pengo hilo. Akizungumza na shirika la habari la China, Xinhua, mkurugenzi mkuu wa kampuni ya ubia ya reli ya SGR ya Ethiopia na Djibouti Tilahun Sarka amepongeza pendekezo linaloendelea la usafirishaji ujuzi linalolenga kuongeza uwezo wa wasomi vijana wa Ethiopia na Djibouti katika sekta ya reli.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako