• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanajeshi wanne wajeruhiwa katika shambulizi la roketi dhidi ya kituo cha jeshi mkoani Salahudin, Iraq

  (GMT+08:00) 2020-01-13 09:02:24

  Wanajeshi wanne wa jeshi la anga la Iraq wamejeruhiwa kwenye shambulizi la roketi dhidi ya kituo cha kijeshi cha Balad mkoani Salahudin, katikati ya Iraq.

  Taarifa iliyotolewa na ofisa habari wa Kamandi ya Operesheni za Pamoja ya Iraq imesema kuwa maroketi manane aina ya Katyusha yalianguka katika kituo hicho, ambacho awali kilitumiwa na Jeshi la Marekani, kilomita 90 kaskazini mwa Baghdad, na kuwajeruhi maofisa wawili na askari wawili. Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuwajibika na shambulizi hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako