• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kiongozi mkuu wa Iran ahimiza kupanua ushirikiano wa kikanda

  (GMT+08:00) 2020-01-13 09:38:31

  Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amehimiza kupanua ushirikiano wa kikanda kati ya nchi za eneo la mashariki ya kati.

  Akikutana na kiongozi mkuu wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani, Ayatollah Khamenei amesema, hali iliyopo imeonesha haja ya kuhimiza ushirikiano wa kikanda na kupunguza utegemezi kwa wageni, pia ametoa wito kuongeza ushirikiano wa kiuchumi kati ya pande hizo mbili.

  Sheikh Al-Thani amesema Qatar inakubali kuongeza ushirikiano wa kikanda na kutarajia kufanya mazungumzo kati ya nchi za kanda hiyo. Pia ameshukuru uungaji mkono wa Iran kwa wakati Qatari ilipowekewa vikwazo na baadhi ya nchi za kiarabu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako