• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Real Madrid yainyuka Atletico Madrid 4-1 kwenye penalti na kuondoka na Super Cup la Hispania

  (GMT+08:00) 2020-01-13 10:29:28

  Chereko chereko na nderemo jana zilitawala baada ya timu ya Real Madrid kunyanyua kombe la Super Cup la Hispania kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2017. Real Madrid iliinyuka Atletico Madrid 4-1 katika kipindi cha kupigiana mikwaju baada ya muda wa kawaida na ziada kumalizika wakiwa na sare tasa na kunyakua kombe hilo katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa King Abdullah Sports City huko Jeddah Saudi Arabia. Waliongizia mikwaju Madrid ni Dani Carvajal, Rodrygo, Luka Modric na Sergio Ramos. Na kwa upande Atletico waliokosa penalti zao ni Saul Niguez na Thomas Partey na kuifanya Madrid iondoke kwa shangwe uwanjani. Real Madrid ilimaliza mchezo ikiwa na wachezaji 10 baada ya Federico Valverde kurambwa kadi nyekundu kwa kumfanyia dhambi Alvaro Morata.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako