• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Kipruto, Chepkirui wavunja rikodi ya dunia ya mbio za km 10 huko Valencia

  (GMT+08:00) 2020-01-13 10:30:09

  Mwanariadha wa Kenya anayeshikilia medali ya shaba kwa mbio za mita 10,000 duniani Rhonex Kipruto na bingwa wa mbio za m 5,000 mwaka 2016 wa Afrika Sheila Chepkirui wameweka rikodi za dunia kwenye mbio za km 10 kwa wanawake na wanaume huko Valencia, Hispania. Kipruto mwenye miaka 20 jana alishinda mbio hizo za barabarani za Valencia Ibercaja km 10 na kuandikisha rikodi mpya duniani ya dakika 26 na sekunde 23. Rikodi hiyo ameivunja wiki sita tu baada ya bingwa wa dunia wa mita 10,000 Mganda Joshua kuiweka katika mbio za nusu marathoni zilizofanyika Disemba mosi huko Valencia. Naye Chepkirui, aliyepata medali ya fedha katika mbio za nyika za Afrika mwaka 2016 amerejea na kuweka rikodi mpya ya dakika 29:42 kwa upande mbio za wanawake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako