• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake U 17 yainyeshea mvua ya magoli 5-1 timu ya Burundi

  (GMT+08:00) 2020-01-13 10:30:25

  Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake chini ya miaka 17 jana Januari 12 iliimiminia mvua ya magoli 5-1 timu ya Burundi kwenye mchezo wa kuwania kufuzu tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa Wanawake. Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar, ulishuhudiwa na mashabiki wengi waliojitokeza kuipa sapoti timu hiyo ambayo imecheza soka ya pasi nyingi na kushambulia. Mshambuliaji wa Tanzania Asha Masaka alikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Burundi na mlinda mlango wao, Amissa Inarukundo ambaye aliokoteshwa nyavuni mabao matatu ya Asha huku Joyce Meshack na Protasia Mbunda wakipachika bao mojamoja na kukamilisha jumla ya mabao matano kwa vijana wa Tanzania. Bao pekee la kufuta machozi kwa Burundi lilipachikwa na Nadine Ndayishimiye kutokana na uzembe wa safu ya ulinzi wa timu ya Taifa ya Tanzania, U 17. Michuano hiyo inatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu nchini India na mchezo wa marudio unatarajiwa kufanyika Januari 25, nchini Burundi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako