• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mji wa Yiwu nchini China wapanga kuongeza safari za treni za mizigo kwenda Ulaya mwaka 2020

  (GMT+08:00) 2020-01-13 16:33:23

  Mji wa Yiwu ulioko mashariki mwa China ambao unaongoza duniani kwa soko la bidhaa ndogondogo, unapanga kufanya safari 1000 za treni za mizigo kwenda Ulaya kwa mwaka huu, ikiwa ni karibu ya mara mbili zaidi ya zile za mwaka jana.

  Huduma ya usafiri wa treni kati ya China na bara la Ulaya imeendelea kwa kasi mjini Yiwu tangu ilipoanzishwa mwaka 2014. Mwaka jana, safari 528 za treni za mizigo zilifanywa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 65 ikilinganishwa na mwaka 2018.

  Huduma hiyo sasa ina njia 11 ikiunganisha mji wa Yiwu na nchi na sehemu 37 katika bara la Asia na Ulaya. Mji huo pia umeshuhudia biashara kubwa na chi zilizo kwenye Ukanda Mmoja na Njia Moja, huku biashara ya nje ikitarajiwa kuongezeka kwa asilimia 11 kwa mwaka jana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako