• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wang Yi aeleza sababu tatu za kufanya ziara ya kwanza ya kila mwaka barani Afrika kwa miaka 30 mfululizo

    (GMT+08:00) 2020-01-13 16:56:37

    Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye yuko ziarani nchini Zimbabwe, jana amekutana na waandishi wa habari nchini humo akiwa pamoja na mwenyeji wake, Sibusiso Moyo.

    Akijibu kwa nini waziri wa mambo ya nje wa China hufanya ziara ya kwanza ya kila mwaka barani Afrika kwa miaka 30 mfululizo, Wang Yi amesema, ni kwa sababu ya hisia maalumu ya urafiki wa kizazi baada ya kizazi na kukabiliana na taabu kwa pamoja kati ya China na Afrika, pia ni kwa sababu ya mahitaji halisi ya kuzidisha ushirikiano na kuendeleza kwa pamoja. Lakini pia, Wang Yi amesema desturi hiyo inafanyika kutokana na majukumu muhimu ya kuimarisha uratibu wa kimataifa na kulinda maslahi ya pamoja.

    Bw. Wang Yi amesema, China itaendelea na desturi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako