• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kakamega Homeboyz yachapa Gor Mahia 2-1 na kupata raha ya kushinda nyumbani

  (GMT+08:00) 2020-01-13 17:06:27

  Hatimaye Kakamega Homeboyz wamepata ushindi wao wa kwanza dhidi ya Gor Mahia baada ya kuwachabanga 2-1 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Bukhungu hapo jana. Shami Kibwana na Ali Bai wameifungia Kakamega Homeboyz mabao hayo ya ushindi huku wakiwa na hamu ya kushinda taji la Ligi Kuu ya Kenya. Nicholas Kipkirui ndiye aliwafungia mabingwa hao wa KPL bao la pekee katika Kaunti ya Kakamega. Kakamega Homeboyz walionekana kikosi bora katika awamu ya kwanza lakini walishindwa kutumia nafasi hiyo kufunga mabao. Iliwachukuwa wenyeji hao dakika 20 kupenya katika ngome ya K'Ogalo na kufunga bao la kwanza kupitia kwa Kibwan. Gor Mahia walisawazisha bao hilo kupitia kwa Kipkirui ambaye alitumia kichwa kuonja wavu dakika ya 40.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako