• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Simba, Mtibwa nani mfalme kombe la Mapinduzi leo?

  (GMT+08:00) 2020-01-13 17:06:49

  Simba na Mtibwa leo zinakutana kwenye fainali ya 14 kombe la Mapinduzi, mchezo ambao unaendela hivi sasa katika uwanja wa Amaan. Timu hizo zilifikia hatua ya fainali baada ya kushinda katika michezo yao, ambapo Mtibwa iliwafunga Yanga kwa penalti 4-2 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90, Simba iliitoa Azam FC kwa penalti 3-2 baada ya dakika 90 kutoka sare ya bila ya kufungana. Mashindano hayo yalianza kutimua vumbi Januari 6 ambapo jumla ya timu nane zilishiriki nne kutoka Zanzibar na nne kutoka Tanzania bara, ambapo msimu huu zilichezwa kwa njia ya mtoano. Mchezo huo wa fainali unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote kwani kila timu ina historia nzuri ya mashindano hayo, hadi sasa Mtibwa imeingia fainali mara tano na kufanikiwa kutwaa kombe hilo mara moja mwaka 2010 ilipoifunga Ocean View.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako