• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatumai kutatua kwa njia mwafaka suala la Iran kuangusha ndege ya abiria kwa makosa

  (GMT+08:00) 2020-01-13 17:20:37

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema, China inasikitika kuhusu ajali ya ndege ya abiria ya Ukraine, na inatumai tukio hilo litatatuliwa kwa njia mwafaka na kuepusha hali hiyo isiwe na utatanishi zaidi.

  Habari zinasema, ndege ya abiria ya shirika la ndege la Ukraine ilianguka wiki iliyopita mara baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Tehran, nchini Iran. Hivi karibuni, Iran ilikiri kuangusha ndege hiyo kwa makosa.

  Bw. Geng Shuang amesema, kutokana na pande husika kuwasiliana kuhusu tukio hilo, China inatumai litatatuliwa kwa njia mwafaka na kuepusha mvutano zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako