• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vikosi vya wapinzani vya Libya vyasaini makubaliano ya kusitisha mapigano mjini Moscow

  (GMT+08:00) 2020-01-13 18:59:55

  Serikali ya Libya imesema vikosi vya wapinzani vya nchi hiyo vimesaini makubaliano ya kusitisha mapigano huko mjini Moscow, nchini Russia.

  Serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya (GNA) imetoa taarifa ya kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kuanzia usiku wa tarehe 12 mwezi huu, saa kadhaa baada ya vikosi vya wapinzani kutangaza kusimamisha mvutano.

  Mvutano wa Libya ulianzia mwaka 2014, na kugawanya madaraka kati ya serikali mbili za wapinzani, serikali ya umoja wa kitaifa inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, na serikali yenye makao yake Tobruk inayoshirikiana na Jeshi la kitaifa la Libya likiongozwa na Jenerali Khalifa Haftar.

  Ripoti zinasema, tayari Jenerali Haftar amewasili mjini Moscow, na anatarajiwa kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Libya Bw. Fayez al-Sarraj atakayewasili Russia hii leo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako