• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkoa wa Xinjiang wawapokea watalii zaidi ya milioni 200 mwaka 2019

  (GMT+08:00) 2020-01-13 19:05:51

  Habari kutoka mkutano wa tatu wa bunge la 13 la umma la mkoa wa Xinjiang, China, zimesema mkoa huo umepokea watalii zaidi ya milioni 200 mwaka 2019, na pato lililotokana na utalii mkoani humo lilifikia dola zaidi ya bilioni 50 za kimarekani.

  Mkuu wa mkoa wa Xinjiang Bw. Shohrat Zakir amewasilisha ripoti ya kazi za serikali kwenye mkutano huo akisema, mwaka 2019, mkoa huo ulitekeleza mkakati wa kustawi kwa kupitia utalii, kuhimiza kwa nguvu maendeleo ya sekta ya utalii mkoani humo, kuhimiza mafungamano ya sekta za utamaduni na utalii, kuongeza na kuboresha vifaa vya utalii, na kuboresha ubora wa huduma.

  Mjumbe wa bunge la umma la mkoa huo Bw. Miao Xinzhuo amesema, maendeleo ya sekta ya utalii ni matokeo ya utulivu wa hali ya uchumi na jamii, sekta ambayo inahimiza maendeleo ya vyakula, hoteli na nyinginezo, pia inahimiza ongezeko la nafasi za ajira moja kwa moja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako