• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hakuna jambo lolote linaloweza kuzuia maendeleo ya ushirikiano wa kimataifa juu ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

  (GMT+08:00) 2020-01-13 19:06:23

  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesisitiza kuwa, hakuna nchi yoyote inayokwama kutokana na madeni kufuatia uwekezaji wa China.

  Geng amesema, shaka au kashfa yoyote dhidi ya pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" haitazuia maendeleo ya ushirikiano wa kimataifa juu ya pendekezo hilo. Hadi sasa, China imesaini makubaliano 199 ya ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na nchi 137 na mashirika 30 ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na nchi 44 za Afrika na kamati ya Umoja wa Afrika. Hii inaonyesha jumuiya ya kimataifa na Afrika zinavyounga mkono pendekezo hilo, pia ni jibu mwafaka dhidi ya kauli zenye nia mbaya.

  Ameongeza kuwa kwa sasa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yuko ziarani barani Afrika, na nchi anazotembelea katika bara hilo zinasifu sana ushirikiano wa kimataifa juu ya pendekezo hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako