• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ushirikiano kati ya China na Afrika utachangia maendeleo ya dunia katika mwaka mpya

  (GMT+08:00) 2020-01-13 19:45:23

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amefanya ziara katika nchi tano barani Afrika kuanzia tarehe 7 hadi 13 mwezi huu, na nchi alizotembelea ni pamoja na Misri, Djibouti, Eritrea, Burundi na Zimbabwe.

  Katika miaka 30 iliyopita, waziri wa mambo ya nje wa China hufanya ziara ya kwanza ya kila mwaka barani Afrika. Kama Bw. Wang Yi alivyosema, kitendo hicho kinatokana na urafiki kati ya pande hizo mbili kizazi baada ya kizazi, na hisia maalumu kutokana na kukabiliana kwa pamoja na matatizo mbalimbali, vilevile kutokana na mahitaji ya kukuza ushirikiano na kupata maendeleo pamoja, na majukumu muhimu ya kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na kulinda maslahi ya pamoja.

  Mwaka 2020 ni muhimu kwa uhusiano kati ya China na Afrika. Huu si kama tu ni mwaka wa 20 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, bali pia ni mwaka wa 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na nchi za kijadi za uhusiano wa kirafiki zikiwemo Ghana na Mali. Lengo la ziara ya Bw. Wang Yi kufanyika wakati huu maalumu ni kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa kati ya viongozi wa China na Afrika, na matokeo yaliyopatikana katika mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, ili kusukuma mbele ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kukuhimiza uhusiano kati ya China na Afrika kupata maendeleo mapya.

  Kutokana na mtizamo wa dunia, China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, na Afrika ni bara linalojumuisha nchi nyingi zaidi zinazoendelea, kuimarisha ushirikiano kati ya pande hizo mbili kutachangia katika kulinda maendeleo na utulivu wa dunia. Katika miaka ya hivi karibuni, utaratibu wa upande mmoja na siasa za umwamba umekuwa ukifufuka, hali ambayo imeathiri vibaya nchi mbalimbali zinazoendelea duniani zikiwemo nchi za Afrika. China na Afrika zinahitaji sana kuimarisha mawasiliano na uratibu, kuonesha nguvu ya kuwa na umoja, na kutoa sauti ya pamoja. Kama katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alivyosema, mafanikio ya Afrika yana umuhimu mkubwa kwa amani na maendeleo ya dunia, wakati ushirikiano na China una umuhimu mkubwa kwa mafanikio ya Afrika.

  Wakati wa ziara hiyo, Bw. Wang Yi amesisitiza kuwa, China inashikilia kutoingilia mambo ya ndani ya nchi za Afrika, kutoweka masharti ya kisiasa, kusikiliza sauti za Waafrika, kuheshimu matakwa ya Afrika na kukidhi mahitaji ya Afrika.

  Ziara ya Bw. Wang Yi barani Afrika ilikaribishwa kwa shangwe na waafrika, hivyo imeonesha kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika katika mwaka mpya utakuwa na matumaini makubwa, na uhusiano kati ya pande hizo mbili utapata fursa mpya za maendeleo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako