• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ethiopia imeondoa ushuru unaotozwa usafirishaji wa bidhaa za ngozi

  (GMT+08:00) 2020-01-13 20:06:52
  Wizara ya Biashara na Viwanda ilitangaza kwamba Ethiopia imeondoa ushuru unaotozwa kwa usafirishaji wa bidhaa za ngozi tangu Januari 06/2020 ili kuokoa sekta hiyo.

  Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Waziri wa Jimbo Teka Gebreyesus amesema kuwa utekelezaji wa ushuru wa usafirishaji wa bidhaa za ngozi zilizomalizika umeathiri vibaya Sekta hiyo.

  Wakati huohuo Teka alibaini kuwa kodi iliyowekwa katika sekta hiyo ilikuwa kubwa na kusema ndio sababu kuu ya kuanguka kwa sekta hiyo, serikali sasa imeamua kuondoa ushuru kwa bidhaa za ngozi .

  Rais wa chama cha ngozi Ethiopia Berhanu Abate ,amelibaini kuwa ingawa ngozi inapendwa zaidi ushuru ulionekana kuwa hatari kwa utendaji kazi wa sekta hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako