• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Zimbabwe akutana na waziri wa mambo ya nje wa China

  (GMT+08:00) 2020-01-13 21:12:04

  Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe leo amekutana na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi.

  Rais Mnangagwa amesema Zimbabwe inashukuru China kwa kuipatia nchi hiyo msaada kwa maendeleo ya uchumi na jamii, na anatumai China itaendelea kuisaidia Zimbabwe kuharakisha mageuzi ya uchumi na kutimiza maendeleo. Amesema Zimbabwe inashikilia sera ya kuwepo kwa China moja, na itaendelea kuunga mkono China katika masuala yote yanayohusiana na maslahi makuu ya China. Zimbabwe pia inatumai kutumia fursa ya kuadhimisha miaka 40 tangu nchi hizo mbili kuanzisha uhusiano wa kibalozi, kuzidisha hali ya kuaminiana kati yake na China na kuinua kiwango cha ushirikiano.

  Bw. Wang Yi amesema, China inaunga mkono Zimbabwe kufanya juhudi katika kulinda mamlaka ya nchi na heshima ya kitaifa, inaiunga mkono kuchagua yenyewe njia ya kujiendeleza, na kutetea kuondoa vikwazo visivyo vya haki dhidi yake kwa haraka. Pia amesema, China inapenda kufanya uaminifu kati ya nchi hizo mbili uwe nguvu wa ushirikiano kati ya pande mbili, na kutumia ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na FOCAC, kuhimiza miradi mingi zaidi kutekelezwa na kunufaisha watu wa nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako