• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zambia asema haikubaliki kwa watu wa nje kuamuru utawala wa Afrika

    (GMT+08:00) 2020-01-14 08:58:14

    Rais Edgar Lungu wa Zambia amesema haikubaliki kwa watu wa nje kuamuru jinsi nchi za Afrika zinavyopaswa kuongozwa. Rais Lungu amesema, Afrika inapaswa kuruhusiwa kuamua jinsi inavyojitawala badala ya kuamirishwa na watu wa nje.

    Amesema Afrika imekuwa inachagua pole pole jinsi watu wake wanavyoongozwa, na muundo gani wa utawala au taasisi gani zitawekwa.

    Rais Lungu amesema hayo akikutana na balozi wa Sudan Award Ali anayemaliza muda wake nchini Zambia, na kusema serikali yake itaendelea kushirikiana na mashirika yote ya kikanda barani Afrika. Rais Lungu pia ameahidi kukuza uhusiano kati ya Zambia na Sudan, ili kuboresha maisha ya watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako