• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanasayansi wa China na Kenya kufanya utafiti wa kibaiolojia ziwa la Turkana

    (GMT+08:00) 2020-01-14 09:04:06

    Wanasayansi wa Kenya na China wanatarajiwa kushirikiana kufanya utafiti wa kibaiolojia katika Ziwa la Turkana, kaskazini magharibi mwa Kenya mwaka huu.

    Mkurugenzi wa kitengo cha zuolojia cha Jumba la Makumbusho la taifa la Kenya NMK Bibi Esther Kioko, amesema mjini Nairobi kuwa mradi wa utafiti wa kibaiolojia wa Ziwa Turkana utakuwa juhudi za pamoja kati ya NMK, Kituo cha utafiti wa pamoja kati ya China na Afrika na Mamlaka ya Wanyamapori Kenya KWS.

    Bibi Kioko amesema hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa utafiti wa pamoja kuhusu wanyama na mimea kufanyika katika eneo la Ziwa Turkana.

    Ofisa huyo pia amesema utafiti huo utaweka jukwaa la kuwajengea uwezo watafiti wa Kenya kutokana na ushirikiano kati yao na wanasayansi wa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako