• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasema watu milioni 8.4 nchini Ethiopia kuhitaji msaada kwa mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2020-01-14 09:33:26

    Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia uratibu wa mambo ya kibinadamu UNOCHA, imesema watu wapatao milioni 8.4 wanakadiriwa kuwa na mahitaji ya msaada wa kibinadamu nchini Ethiopia kwa mwaka huu.

    UNOCHA imetoa ripoti mpya kuhusu mahitaji ya kibinadamu nchini Ethiopia ikisema wengi kati ya watu hao wanaohitaji msaada wako Oromia ambayo ni kanda kubwa zaidi nchini Ethiopia. Ofisi hiyo pia imesema, asilimia 74 hivi ya watu hao milioni 8.4 wamekuwa na mahitaji ya dharura yanayohitaji kutatuliwa mara moja.

    Wakati huohuo, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, limesema linakabiliwa na pengo kubwa la fedha zinazohitajika kukidhi mahitaji ya wakimbizi nchini Ethiopia.

    Shirika hilo limesema, limepata dola milioni 150.3 za kimarekani kati ya ujumla wa dola milioni 346.5 za kimarekani zinazohitajika kukidhi mahitaji ya msingi ya lishe, elimu, afya na makazi ya wakimbizi nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako