• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la UN larefusha muda wa tume yake nchini Yemen kwa miezi 6

    (GMT+08:00) 2020-01-14 09:37:56

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kurefusha muda wa tume yake maalum nchini Yemen kwa miezi 6, ili kuunga mkono makubaliano ya Hodeidah kati ya serikali ya Yemen na kundi la waasi la Houthi.

    Azimio nambari 2505 lililokubaliwa na nchi 15 wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja lilirefusha muda wa tume maalumu wa UN nchini Yemen hadi kufikia tarehe 15 mwezi Julai mwaka 2020.

    Tume maalum ya Umoja wa Mataifa ya kuunga mkono makubaliano ya Hodeidah itaendelea kuongoza na kuunga mkono uratibu na usimamizi wa Umoja wa Mataifa kusimamisha vita mkoani Hodeidah, kusimamisha utumaji wa vikosi na operesheni za kuondoa mabomu ya ardhini, kuhimiza pande zote kusitisha vita na kuhamisha vikosi kutoka mji wa Hodeidah na bandari za Hodeidah, Salif na Ras Issa, kushirikiana na pande zinazopambana ili kikosi cha usalama kilinde utulivu na usalama wa mji na bandari kwa mujibu wa sheria za Yemen.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako