• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • 21 wauawa kaskazini magharibi mwa Syria huku makubaliano mapya ya kusimamisha vita yakionekana kuleta ushwari

  (GMT+08:00) 2020-01-14 09:51:00

  Watu 21 wakiwemo watoto wanane na wanawake watano wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kwenye mashambulizi makali ya anga yaliyotokea kaskazini magharibi mwa Syria wikiendi hii. Hata hivyo, makubaliano ya kusimamisha vita yaliyoanza kutekelezwa Jumapili yameripotiwa kuleta utulivu wa kiasi. Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema Umoja huo unazitaka pande zote na wale wenye ushawishi na pande hizo kulinda usalama wa raia na miundombinu ya kiraia, pamoja na majukumu yao kwa mujibu wa sheria ya ubinadamu ya kimataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako