• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sahel G5 na Ufaransa zakubali kuunda jeshi la pamoja kupambana na wapiganaji wenye itikadi kali

  (GMT+08:00) 2020-01-14 10:20:17

  Nchi 5 za Afrika magharibi (Sahel G5) na Ufaransa zimekubali kuunda jeshi la pamoja kupambana na wapiganaji wenye itikadi kali katika eneo la Sahel.

  Taarifa ya pamoja iliyotolewa na marais wa Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania, Niger na Ufaransa imesema, lengo muhimu ni kupambana na kundi la IS katika eneo hilo. Pia zimeihimiza Marekani kuendelea kutoa misaada kwa jeshi lao.

  Rais Emmanuel Macron amesema Ufaransa itatuma askari 220 zaidi kushiriki kwenye operesheni ya Barkhane ambayo imesaidia nchi hizo za Afrika kudumisha utawala na kuzuia uingiliaji wa kundi la IS.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako